SPIKA WA BUNGE LA KAUNTI YA ELGEIYO MARAKWET ATETEA RUZUKU YA MAGARI KWA WAWAKILISHI WA WADI

You are currently viewing SPIKA WA BUNGE LA KAUNTI YA ELGEIYO MARAKWET ATETEA RUZUKU YA MAGARI KWA WAWAKILISHI WA WADI

Spika wa Kaunti ya Elgeiyo Marakwet Philemon Kiplagat Sabulei anasema kwamba ruzuku ya magari kwa Wawakilishi Wadi na maspika wa mabunge ya Kaunti hazina uhusiano wowote na mswada wa marekebisho ya Katiba ya Mwaka wa 2020.

Sabulei amepinga madai kwamba ruzuku ya magari imetolewa kwa Wawakilishi Wadi kama hongo ili kuhakikisha kwamba wanaunga mkono mswada huwo na kuupitisha bungeni.

Anasema Wawakilishi Wadi Kaunti hiyo watajadili na kutoa uamuzi wao baada ya Wananchi kutoa maoni yao pasi na kushawishiwa kisiasa.

Aidha amesema kwamba ruzuku hiyo ya magari ni haki kwa Wawakilishi Wadi ikizingatiwa kwamba kazi wanayofanya inawalazimu kusafiri mwendo mrefu na ilifaa kutekelezwa pindi ugatuzi ulipoanzishwa nchini.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.