Chifu wa Kata ya Sitatunga katika Kaunti ya Trans Nzoia, Joseph Weyele amewawahimiza wafanyabiashara kutundika kamera za CCTV katika majengo yao ili kuimarisha usalama na vilevile kuhifadhi data zinazoweza kutumika kama ushaidi utovu wa usalama unaposhuhudiwa.
Akilirejelea tukio la wizi ambalo Afisa wa polisi wa Akiba, NPR aliyeuliwa kwa kupigwa risasi na genge la majambazi ambalo vilevile lilimjeruhi afisa wa polisi na mwananchi mmoja katika soko la Sibanga kabla kutoweka na kitita cha pesa kisichojulikan, Wayele amesema oparesheni ya kulisaka genge hilo limeanzishwa.
Aidha ametumia fursa hiyo kuwarai wananchi kushirikiana na viongozi wa mpango wa nyumba kumi kuwaripoti watu wanaowashuku kuwa wahalifu ili kuhojiwa na kuajibishwa.