ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI LA ELDORET DOMINIC KIMINGICH AJIBU MADAI YALIYOIBULIWA FACEBOOK KUHUSU OPARESHENI-KAPEDO.

You are currently viewing ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI LA ELDORET DOMINIC KIMINGICH AJIBU MADAI YALIYOIBULIWA FACEBOOK KUHUSU OPARESHENI-KAPEDO.

Askofu wa Jimbo Katoliki la Eldoret Dominic Kimingich amejibu kuhusu taarifa zilizochapishwa na mtumiaji moja wa mtandao wa Facebook aliyedai kuwa hana ruhusa ya kuingilia taratibu za serikali za kuendesha operasheni eneo la Kapedo ikizingatiwa kuwa alishindwa kuzungumzia suala la utovu wa usalama eneo hilo wakati akiwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Lodwar.

Akizungumza mjini Lodwar Kimingich amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote huku akisisitiza kuwa anaunga mkono operasheni inayoendelea Kapedo, akisema kuwa vyombo vya usalama vinapaswa kuendesha operesheni hiyo bila kuwadhulumu wananchi wasiokuwa na hatia.

Hata hivyo Kimmingich ambaye pia ni Msimamizi wa Jimbo katoliki la Lodwar ametoa wito kwa serikali kufungua barabara za kuelekea eneo la Kapedo ili wahisani na washirika wa maendeleo waweze kutoa msaada wa vyakula kwa wakaazi wa eneo hilo ambao kwa njia moja au nyingine wanaweza athirika na njaa kutoka na operesheni ya kiusalama ya kuwasaka wahalifu.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa