Waandaaji wa tuzo za MTV Africa Music Awards wameahirisha hafla za ugawaji wa tuzo hizo zilizokuwa zifanyike Kampala Uganda Februari 20 mwaka huu.
Kwenye taarifa yao, MTV Base wamesema wameahirisha ugawaji wa tuzo hizo za 7 mpaka itakapotangazwa tena huku wakishindwa kutaja sababu iliyopolekea kuahirishwa kwa tuzo hizo.
Tovuti ya CCN imeripoti kwamba Bobi Wine na wafuasi wake wanahusika kwenye sababu za MTV MAMA kuahirishwa kutokana na madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na serikali ya Uganda, madai ambayo yamewasilishwa mtandaoni na Bobi Wine ambaye alikuwa mgombea wa kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.