Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Nicah the Queenn amenyosha maelezo kuhusu video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha akijaribu kuwaalika watu kanisani wikiendi iliyopita.
Kupitia Insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Nicah amesema hakutegemea video hiyo itatrend kwani aliitengeneza bila kukusudia lakini kwa bahati mbaya alishangaa imetrend kwa sababu ya maungo yake ya mwili.
Mkali huyo wa ngoma ya “Ushuhuda” amedai kwamba mwili wake haufai kutambulisha dini lake au kueleza upendo wake kwa Yesu kristo kwani hata akivalia gunia makalio yake yataonekana tu.
Kauli ya Nicah the Queen inakuja mara baada ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii kumtolea uvivu msanii huyo kwa madai ya kuchapisha video hiyo kwa kukusudia ili kuonyesha maungo ya mwili wake huku akiwasilisha ujumbe wa kanisa.