MTANDAO WA INSTAGRAM KUFICHA IDADI YA LIKES.

You are currently viewing MTANDAO WA INSTAGRAM KUFICHA IDADI YA LIKES.
  • Post category:Teknolojia

Instagram inafanya majaribio mengi katika kuboresha mpangilio wake na experience yake ikiwemo kuweka uhuru kwa mtumiaji kuzuia likes zisionekane kwa watazamaji na followers.

Mwenye account pekee yake ndiye ambaye atakuwa na uwezo wa kuona idadi ya likes katika post zake. Katika kufanya marekebisho katika app yake jana ilizuia idadi ya “likes” kuonekana katika post zake kwa masaa machache.

Likes zilikuwa zinaonekana tu kwa mwenye account lakini kwa followers na watazamaji hazionekani. Instagram imesema ilikuwa inafanya majaribio ya kutoa likes kwa baadhi ya watumiaji, lakini kutokana na matatizo ya kiufundi jaribio likawapata watumiaji wengi wakapata mabadiliko hayo kwa bahati mbaya.

Bado Instagram inajaribu kuzuia likes kuonekana kwa baadhi ya watumiaji. Twitter pia ni moja kati ya kampuni inayojaribu kuondoa likes zisionekane kwa sababu inasemekana itasaidia watu kuwa free na wabunifu.

Likes zinafanya watu kuwa na hofu ya kuanzisha mawazo, likes zinafanya watumiaji wanakuwa na drama kutafuta likes na kusahau kuweka focus katika contents. Idadi ya likes bado itabaki lakini zitaonekana na watu wenye account tu.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa