Google imetishia kuondoa kitafutio chake (search engine) nchini Australia huku Facebook ikidai itaondoa maudhui ya habari iwapo sheria mpya ya inayoyataka makampuni hayo yavilipe vyombo vya habari ikipitishwa.
Sheria hiyo iliyopendekezwa na bunge la Australia itawalazimu Facebook na Google kujadiliana malipo na mashirika ya habari ambayo habari zake zinatokea kwenye majukwaa hayo.
Google na Facebook wanadai kuwa sheria hiyo haitatekelezeka na kwamba ni tishio kwa aina ya biashara yao.
GOOGLE YATISHIA KUJIONDOA AUSTRALIA IWAPO SHERIA HII IKIPITA
