Mtandao wa Google imechapisha taarifa mpya katika Blogu yake rasmi na kuelezea kuhusu mabadiliko mapya katika muonekano wake kwenye simu.
Google imesema itaanza kuweka muonekano mpya, ambapo imeweka rangi, subtopics na data nyingi zinaonekana kwa urahisi kabla ya kufungua links. Pia subtopics zinaonekana chini ya sehemu ya ku-search ili kumsaidia msomaji kupata taarifa za aina tofauti kuendana na unachotafuta.
Hii ni moja katika ya mabadiliko ambayo Google ilitangaza kwenye ile hafla ya Search On ambayo Google ilitambulisha mabadiliko mapya yatakayoanza mwaka huu katika tovuti yake.