WhatsApp imekanusha kuhusu kutumia taarifa za chats za watumiaji wake, imesisitiza kuwa WhatsApp inatunza chats za watumiaji wake katika mfumo wa End-to-End encryption ambapo ni mtumaji na mpokeaji wa message peke yake ndio ambao wanaweza kufahamu kilichopo katika chats.
Imekanusha uvumi wa kutumia vibaya na imesema chats za watumiaji zitaendelea kubaki kuwa ni siri. Pia Voice-calls na audio-calls zote ni encrypted na hazihifadhiwi katika servers.
Kwa upande mwingine ni vyema watumiaji wake kufahamu taarifa ambazo WhatsApp itakuwa inakusanya na ku-share na Facebook hazitahusisha taarifa za kwenye chats.
Chats zitaendelea kuwa encrypted na hakuna ambaye ataweza kuzitazama, hata whatsApp yenyewe imesema haiwezi kufahamu kilichopo katika chats.