Chrome imeweka muonekano mpya wa tabs kwa watumiaji wote wa Android. Browser hii inayotumika na watumiaji wengi duniani, imeboresha mpangilio wa tabs.
Tabs ni kurasa za website (tovuti) ambazo umezifungua kwa pamoja, mpangilio mpya wa website zitajipangilia katika style ya Grid lakini pia website ambazo umezifungua kwa pamoja unaweza kuziweka sehemu moja na kutengeneza group.
Ni njia nzuri na mpangilio unaosaidia watumiaji ambao wanafungua browser nyingi kwa pamoja mfano ukiwa unasoma au kuperuzi story moja inayofanana utaweza kufungua website nyingi kwa pamoja na kuzipangilia. Hii ni kwa watumiaji wa Android katika app ya Chrome.