FACEBOOK YAZINDUA APP MPYA INAYOWEZESHA WATUMIAJI KUJIREKODI WAKIIMBA,UWEZO WA KUSOMA LYRICS NA BEATS ZA KUREKODI.

You are currently viewing FACEBOOK YAZINDUA APP MPYA INAYOWEZESHA WATUMIAJI KUJIREKODI WAKIIMBA,UWEZO WA KUSOMA LYRICS NA BEATS ZA KUREKODI.
  • Post category:Teknolojia

Baada ya kuweka Instagram Reels, New Product Experimentation (NPED) timu ya Facebook inayohusika na kutengeneza app za majaribio chini ya kampuni ya Facebook, jana imetoa app mpya ya majaribio.

Facebook imetoa app ya majaribio iliyopewa jina la BARS. Ni app ambayo inawawezesha watumiaji kurekodi video za sekunde 60, kwa kuimba. Ni app ambayo inafanana na TikTok, ina filters, beats za rap, visual filters, sound effects (ina autotunes, sound filters n.k) na uwezo wa kuona lyrics na maneno ambayo unaweza kuyaimba.

Ni app ya majaribio, ambayo ni kama sehemu ya kujaribu kupunguza nguvu ya TikTok. Inafanana na TikTok lakini tofauti yake inawalenga watu wanaopenda kurekodi video za kuimba.

Ni sehemu ya Facebook kujaribu kama inaweza kushika soko la short videos za kuimba. Ina upekee wake kwa kuweka lyrics, beats na sound filters zinazotumika katika production za miziki

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa