Kampuni ya Samsung inatengeneza miwani maalum zilizotengenezwa na mfumo wa Augumented reality (AR) na VR yenye umbo sawa na miwani ya kawaida.
Samsung imetoa video kuonyesha matumizi makubwa ya miwani zake.
Video inaonyesha miwani zenye kioo ambacho kinaonyesha taarifa mbalimbali kama vile documents, videos na apps.
Frame zake ni pana ili kuruhusu sehemu ya battery kujificha na zinaweza kuunganishwa na simu, vifaa vya games (controllers), drones na unaweza kuitumia kama Sunglasses.
Samsung AR Glasses zitakuwa na uwezo mkubwa zaidi, watumiaji wataweza kuchagua vitu hewani bila kutumia kioo. Pia inaweza kuonyesha vitu vya 3D na ukaweza kuvigusa vizuri.
Glasses Lite itakuwa ni toleo la bei ya chini, unaweza kuunganisha na keyboard, saa na simu. Ina uwezo wa kutazama videos, kusoma messages, video calls, na kuitumia kama miwani ya kawaida.
Samsung, Apple, Google, Facebook, Oppo, Lenovo na Microsoft ni kampuni kubwa za teknolojia ambazo kwa sasa zinapambana kutengeneza miwani zenye uwezo wa AR na VR.
Inategemewa miwani-janja (smart-glasses) zinategemewa sana kubadilisha soko la simu kwa sababu itakuwa ni rahisi na zina uhalisia kuzitumia kuliko simu.