Kampuni ya Apple itaacha kuuza na kutengeneza iMac Pro, lakini itaendelea kuipatia updates kama kawaida. iMac Pro ni toleo la iMac mwaka 2017, ilikuwa na inch 27 na muonekano wake ulitrend sana baada ya Apple kuweka kioo cha iMac kuwa chembamba.
Mwaka huu Apple inategemewa kufanya mabadiliko makubwa ya iMac zake (Desktops za Macs); inategemewa kuweka chip ya M1 na kuboresha muonekano.
Bado iMac itaendelea kupata updates hivyo sio taarifa mbaya sana kwa wale ambao tayari wanaitumia. Kwenye Website ya Apple, imesema baada ya stock iliyopo kuisha, hazitauzwa tena.