Lebo ya muziki ya Firebase Crew Entertainment ya nchini uganda ilipoteza umaarufu mara baada ya Bob wine ambaye ni mmiliki wa lebo hiyo kujiunga na masuala ya siasa.
Tangu wakati huo lebo hiyo haijepata kiongozi dhabiti na wasanii wengi chipukizi chini ya lebo hiyo wanahisi kutengwa.
Sasa hitmaker wa ngoma ya “Ratata” msanii Zex amesema kuwa yeye ndiye mtu sahihi wa kuchugua nafasi ya Bob Wine ikitokea kiongozi huyo wa NUP ataachana na muziki na kujiunga na siasa.
Kulingana na Zex ana muziki mzuri ambao utaisaidia Lebo ya Fire Base Entertainment kurejea kwenye upeo wake kama jinsi ambavyo ilikuwa kipindi cha nyuma chini uongozi wake Bob Wine.
Ikumbukwe Zex alipata umaarufu kwenye kiwanda cha muziki nchini uganda alipoachia single iitwayo “Ratata” kabla ya kuachia single nyingine kali iitwayo “Nalinda.”