Mwanamuziki wa hiphop nchini Octopizzo amefunguka na kusema kuwa yeye hafanyi muziki ili kupata au kushinda tuzo.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter Octopizzo amewataka mashabiki wa muziki wake watambue kuwa yeye hafanyi muziki ili kupata tuzo bali anafanya muziki kutoa burudani, pamoja na kumuingizia kipato, hivyo ndio maana siku zote huwa anajiita mwanamuziki mfanyabiashara.
Kauli hiyo ya Octopizzo imekuja mara baada ya wadau wa muziki nchini kumshinikiza kufanya collabo na wasanii wa kimataifa ili aweze kuteuliwa kushiriki kwenye tuzo kubwa za muziki duniani za BET kwa lengo la kuupeleka muziki wa Kenya kimataifa.