MSANII WA BONGOFLEVA IBRAAH MBIONI KUACHIA ALBUM MPYA.

You are currently viewing MSANII WA BONGOFLEVA IBRAAH MBIONI KUACHIA ALBUM MPYA.
  • Post category:Burudani

Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Ibraah yuko jikoni kwa ajili ya kuiandaa album yake ya kwanza tangu aanze safari yake ya muziki.

Kupitia Instastory yake kwenye mtandao wa instagram meneja wa lebo ya muziki ya konde gang Mjerumani amepost picha ya ibraah akiwa studio na kuandika “Blessed son album n the making”.

Kama album hiyo itatoka itakuwa ni album ya kwanza kwa msanii huyo ambaye tayari alifanikiwa kuachia “EP” ¬†yake inayofahamika kama “Steps” iliyotoka mwaka 2020 .

Sanjari na hilo Ibraah amewaacha mashabiki zake na maswali baada ya kupost picha akiwa na mwanamke wa kizungu bila kuandika chochote.
Watu wengi wanadhani huenda akwa ndiye mpenzi wake mpya kutokana na comments za wanafamilia wenzake wa lebo ya konde gang.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa