Meneja wa zamani wa klabu za West Ham na Newcastle, Glenn Roeder amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 65.
Meneja Roeder alifariki Februari 28 2021 na taarifa za kifo chake zimetangazwa na Chama cha Wasimamizi wa Ligi Kuu Uingereza ‘LMA’.
Meneja huyo raia wa Uingereza alifariki kutokana na maradhi ya uvimbe wa ubongo yaliyomsumbua kwa muda mrefu.
Roeder aliitumikia West Ham kati ya 2001 na 2003, na kupata uzoefu kwa kuzitumikia klabu nyingine zikiwemo Newcastle United, Gillingham, Watford na Norwich City.