MBOSSO KUJA NA WIMBO MWINGINE WA MAPENZI “DEFINATION OF LOVE”

You are currently viewing MBOSSO KUJA NA WIMBO MWINGINE WA MAPENZI “DEFINATION OF LOVE”
  • Post category:Burudani

Msanii kutoka lebo ya WCB Mbosso ameonekana akikesha studio siku za hivi karibuni na wazalishaji wa muziki mbalimbali akiwemo Lizer Classic na Mocco Genius huenda wimbo au nyimbo alizokuwa busy kuziandaa zipo tayari kwaajili ya kuwapa mashabiki zake waburudike nazo.

Mbosso amekuwa akiaminika sana kwa umahiri wake wa uandishi wa nyimbo za mapenzi, sasa kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram ameandika “Definition Of Love” jambo lililotafsiriwa huenda ikawa ndio jina la kazi yake au kazi zake zinazokuja kwa kuwa msanii huyo amekuwa akiachia nyimbo nyingi za mapenzi.

Ikumbukwe Mbosso hajaachia kazi yoyote kwa mwaka 2021,kazi ya mwisho kutoka kwa msanii huyo ilikuwa ni “Fall” aliyoiachia Novemba 21 mwaka 2020 kwa hivyo watu wakae mkao wa kula muda wowote chakula kinafika.  

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa