Msanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka lebo ya WCB Mbosso ameizungumzia album yake mpya ya Defination of Love ambayo tayari imekamilika.
Hitmaker huyo wa ngoma ya Fall ameeleza kuwa album yake inahusu mapenzi tu na itakuja kuwafundisha watu nini maana ya mapenzi.
Aidha amedai kuwa album hiyo itawahusu waliotendwa, waliopo kwenye mapenzi ya furaha,wanaotaka kuingia kwenye mapenzi lakini pia walioachana na ambao hawapo kwenye mapenzi.
Defition of love itakuwa album ya kwanza ya Mbosso na itaachiwa rasmi Februari 14 mwaka huu ikiwa inahisiwa kuwa huenda ikawa na jumla ya ngoma 10 za moto.