MAYWEATHER AKUBALI OMBILI LA KUZICHAPA NA RAPA 50 CENT.

You are currently viewing MAYWEATHER AKUBALI OMBILI LA KUZICHAPA NA RAPA 50 CENT.
  • Post category:Burudani

Bondia Floyd Maywether kutoka nchini Marekani amekubali ombi la rapa 50 Cent ambaye wiki iliyopita alitangaza kutaka kuzichapa na bondia huyo maarufu mwenye uzito wa Kilo 68.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, alipokuwa akitoa taarifa ya kuahirishwa kwa pambano lake na bondia Logan Paul ambalo lilikuwa lifanyike Februari 20 mwaka huu, Mayweather amesema kwamba amekubali ombi la kuzichapa na rapa 50 Cent, na kama yupo tayari basi wafanye pambano la maonyesho maarufu kama exhibition mwishoni mwa mwaka huu.

Hata hivyo baada bondia huyo kuweka hilo wazi 50 cent aliibuka kupitia mtandao wake wa Instagram na kuweka ujumbe wa utani kuwa pambano lake na Floyd Mayweather limesitishwa kutokana na bondia huyo kushindwa kusoma sentensi mbili za kitabu chake cha “Hustle harder Hustle Smarter”.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa