Staa wa muziki nchini Uganda Cindy Sanyu amewatolea uvivu wasanii ambao wanadhani kwamba muungano wa wanamuziki nchini Uganda ni jukwaa ambalo litawasaidia kiuchumi.
Akiwa kwenye moja ya interview Cindy amesema muungano huo sio shirika la misaada bali ni vuguvugu ambalo litawaleta pamoja wasanii ili wawe na sauti moja ya kutetea muziki wa Uganda.
Hata hivyo amesema wasanii wengi nchini Uganda hawana furaha kwa sababu muungano wa wasanii nchini humo hautoi misaada kwa wasanii, hivyo wasitegemee chakula yeyote kutoka kwake iwapo atachaguliwa kuwa rais wa muungano huo.
Ikumbukwe Cind Sanyu ambaye ni naibu rais wa muungano wa wanamuziki nchini Uganda, kwa sasa ametia nia ya kugombea kiti cha urais wa muungano huo.