Baada ya mrembo anayefahamika kwa jina la Dee kudai kwamba ana uja uzito wa staa wa muziki nchini Willy Paul.
Sasa baadhi ya mashabiki wa msanii huyo wamejitokeza na kukanusha madai yaliyoibuliwa na mrembo huyo.
Wakiongozwa na mwanadada maarufu mitandaoni aitwaye Manzi wa Kibera wamesema tuhuma hizo hazina ukweli wowote ila mrembo huyi anajaribu kulitumia jina la Willy Paul kujitafutia umaarufu.
Kauli ya mashabiki wa willy Paul inakuja baada ya mrembo kwa jina Dee kudai kuwa Willy Paul alimpa ujauzito na kisha akamkimbia, hivyo amehamua kuweka suala hilo wazi ili mtoto wake mtarajiwa apate matunzo kutoka kwa msanii huyo.