MAGOHA: MIKAKATI YAWEKWA KUZUIA UDANGANYIFU KWENYE MITIHANI YA KCPE NA KCSE.

You are currently viewing MAGOHA: MIKAKATI YAWEKWA KUZUIA UDANGANYIFU KWENYE MITIHANI YA KCPE NA KCSE.

Wizara ya Elimu imeweka mikakati ya kutosha kuhakikisha visa vya udanganyifu vinathibitiwa wakati wa mitihani ya  kitaifa nchini.

Kulingana na Waziri wa Elimu Prof. George Magoha mtihani wa KCPE utaanza Machi 22 hadi 24 huku mtihani rasmi kwa wanafunzi wa kidato cha nne ukianza tarehe 26 mwezi Machi na kutamatika Aprili 21.

Aidha Magoha mewaonya maafisa watakaopewa jukumu la kusimamia mitahini hiyo kwamba yeyote atakayehusika katikamvisa vya udanganyifu ataadhibiwa kisheria.

Wakati huo huo Afisa mkuu mtendaji wa Tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC Nancy Macharia anasema makamishna wa kaunti na manaibu wao watahusika pakubwa kuhakikisha mtihani huwo unalindwa ,huku akiongeza kuwa maafisa wote wa elimu katika ngazi ya kaunti  ambao wapo kwenye likizo  wanapaswa kurejea kazini mara moja.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa