LIL WAYNE AMSHUKURU TRUMP 

You are currently viewing LIL WAYNE AMSHUKURU TRUMP 
  • Post category:Burudani

Rapa kutoka Marekani Lil Wayne amechukua wasaa mfupi kuandika ujumbe wa shukrani kwenda kwa Rais mstaafu wa Marekani Donald Trump baada ya kusamehewa makosa yake.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Weezy amemshukuru Trump kwa kupitisha msamaha katika kesi yake ya makosa ya kumiliki silaha kinyume cha sheria ambayo ingempeleka gerezani kwa miaka 10.

Sanjari na hilo rapa mweza KodakBlack ambaye naye alisamehewa na Rais Trump amemshukuru kupitia ukurasa wake wa instagram na ripoti zinasema tangu jana Kodak ameachiwa huru, licha ya vuguvugu la kesi yake mpya ya makosa ya kingono kuibuka.

Ikumbukwe, Trump aliwasamehe watu takribani 70 wakati wa kuachia madaraka yake katika msamaha wa Rais ambapo wasanii hao pia walipata nafasi hiyo ya kusamehewa na kufutiwa makosa yao.  

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa