Rapper Mkanada maarufu kama Drake ameweka rekodi mpya na ya kipekee ya kuwa msanii wa kwanza Duniani kwenye historia ya mtandao wa kusambaza muziki Duniani wa ‘Spotify’ kwa kufikisha streams Bilioni 50+ kupitia kazi zake kwenye mtandao huo.
Drake ambaye jina lake kamili ni Aubrey Drake Graham, anaandika rekodi hii mpya kupitia mtandao wa Spotify kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ukurasa ‘Chartdata’ kwenye mtandao wa twitter, Januari 17 2021.
Vile vile Drake anayetarajia kuongeza Streams zaidi kwenye rekodi yake hii kwenye mtandao huo pale atakapiachia rasmi Album yake ya 6 itakayokwenda kwa jina ‘Certified Lover Boy’ inayotarajiwa kuingia sokoni mapema Mwaka huu.