Aliyekuwa member wa kundi la Kansoul, Kid Kora amefunguka kwa mara ya kwanza sababu za kujiondoa kwenye kundi hilo miaka minne iliyopita.
Kora ambaye aliacha kutumia jina “Kid” kwenye shughuli zake za kimuziki amedai kwamba members wenzake ambao ni Mejja na Madtraxx walikuwa wanamtumia vibaya lakini pia walimzuia kufaidi na miraba au royalties ya nyimbo zao.
Kora alienda mbali sana na kuwachana members wenzake Mejja na Madtraxx kwa hatua ya kukataa kubadilisha maudhui ya nyimbo zao ambayo amedai kwamba ilikuwa inawavunjia wanawake heshima.
Ikumbukwe Rapa huyo mwenye umri wa miaka 34 amekuwa na kundi la Kansoul kwa miaka saba kabla ya kujiondoa mwaka wa 2018 na tangu kipindi hicho hakutoa sababu ya kujitenga kwake.
Mejja,Madtraxx na Kora walipata mafanikio makubwa kama kundi la Kansoul kwani licha ya kuachia singles kali walifanikiwa pia kuteuliwa kushiriki kwenye tuzo za MTV Africa Music kupitia kipingele cha Listeners Choice.