KENYA INATARAJIA KUPOKEA DOZI MILIONI 24 ZA CHANJO YA UGONJWA CORONA.

You are currently viewing KENYA INATARAJIA KUPOKEA DOZI MILIONI 24 ZA CHANJO YA UGONJWA CORONA.

Kenya inatarajia kupokea dozi milioni 24 za chanjo ya ugonjwa Corona iliyotengenezwa na kapuni ya Astrazeneca na chuo kikuu cha Oxford mwezi ujao, kulingana na shirika la habari la Reuters.

Waziri wa Afya nchini Mutahi Kagwe amesema kuwa chanjo hizo ziliagizwa kupitia mpango wa Umoja wa Afrika. Waziri wa mambo ya nje Uingereza, Dominic Raab, ambaye yuko nchini humo kwa ziara ya siku moja, amenukuliwa akisema Uingereza ilikuwa inasaidia Kenya kujitayarisha kuanza kutoa chanjo hiyo.

Kenya ina idadi ya watu takriban milioni 48, kulingana na takwimu ya idadi ya watu mwaka 2019. Na hadi kufikia sasa nchi hiyo imethibitisha maambukizi 99,308 ya virusi vya corona huku watu 1,130,707 wakifanyiwa vipimo vya virusi hivyo.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa