Wizara ya afya katika kaunti ya Trans-Nzoia imeanza mpango wa kuwapa chanjo ya COVID-19 wahudumu wa afya,
Hii ni baada ya kaunti hiyo kupokea dozi 6000 chanjo hiyo, katika mpango ambao pia unawalenga maafisa wa usalama.
Akipokea chanjo hiyo gavana Patrick Khaemba amedokeza kwamba serikali yake itahakikisha kwamba wanaohitaji chanjo hiyo wanapata ili kukabili kuenea kwa maradhi ya COVID-19.
Kwa upande wake kamishna wa kaunti ya Trans-Nzoia Sam Ojwang amewaonya wananchi ambao wanaendelea kupuuza masharti yaliyowekwa kukabili Corona akisema watachukuliwa hatua kali za kisheria.