Mswada wa marekebisho ya katiba mwaka wa 2020 inatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge la kaunti ya Nandi hapo kesho kabla ya kuelekezwa kwa wananchi mashinani.
Spika wa bunge la kaunti ya Nandi Joshua Kiptoo amesema kuhusishwa kwa wananchi kuna manufaa makubwa kuelekea kufanikisha mchakato wa katiba kufanyiwa marekebisho nchini.
Kiptoo amesema bunge hilo litaangazia pakubwa maoni yanayotolewa na wananchi kabla ya kuafikia uamuzi wa kupasisha au kuangusha mswada huo.