Kaunti ya Baringo kwa ushirikiano na wakfu wa Safaricom umefungua rasmi kituo kipya cha utegemezi wa kuwahudumia kina mama na watoto wachanga katika hospitali ya kaunti ya Baringo kilichojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 11, mpango ambao utaboresha upatikanaji wa huduma bora za afya ya mama na mtoto
Kufunguliwa kwa kituo hicho sasa kutawezesha ongezeko la vitanda nane hadi 36 kuimarisha huduma za afya katika kaunti hiyo
Kwa mjibu wa Rita Okuthe ambaye ni mdhamini wa Kampuni ya safaricom amesema wakfu huo umejitolea kufanya kazi na kaunti ya baringo ili kuboresha maisha ya akina mama na watoto katika kaunti hiyo.
Ikumbukwe kuwa mwaka uliopita wakfu wa safaricom ulifanikisha ujenzi wa kituo cha afya cha Barwessa na hospitali ndogo ya Chemolingot kwa gharama ya shilingi milioni 21.