Kampuni ya Nickelodeon imeweka orodha ya majina ya watu walioteuliwa kuwania tuzo za Nickelodeon Kids Choice Awards mwaka 2021.
Mchekeshaji mdogo wa kike kutoka nchini Nigeria, emanuella, mwanadada Elsie Majimbo wa humu nchini na vijana kutoka nchini Uganda Ghetto Kids ni miongoni mwa waliochaguliwa kuwania tuzo hizo mwaka huu.
Orodha ya washiriki wa kuwania tuzo za Nickelodeon Kids Choice Awards mwaka 2021 imewekwa wazi na kampuni hiyo kupitia tovuti yao ambapo tayari watu wameanza kupiga kura kupitia tovuti hiyo hiyo KidsChoiceAwards.com
Tuzo hizo zitatolewa ifikapo Machi 13, na zoezi zima litaonyeshwa katika channel za waandaji wa tuzo hizo pamoja na programu ya matangazo ya moja kwa moja katika vifaa vya iPad, iPhone, na Android kwa wakazi wa nchini Marekani.