Staa wa muziki kutoka nchini Marekani Bow Wow ametangaza vitu ambavyo atajikita navyo baada ya kuachana na muziki.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter rapa huyo amesema atajikita kwenye utengenezaji filamu na vipindi vya televisheni lakini pia atajiunga na mchezo wa Mieleka maarufu kama Wrestling chini ya kampuni ya WWE.
Aidha ameenda mbali zaidi na kumtaja mwana masumbwi Rey Misterio kuwa mshirika wake kisha akasema yupo tayari kushindana na yeyote yule kuwania mkanda wa Tag Team.
Bow Wow ni rapa,mwigizaji na mtangazaji kutoka nchini marekani na alianza kujihusisha na mambo ya muziki mwaka wa 1993 na mpaka sasa ana album zaidi ya 15 tangu aanze muziki.