Rapa Tekashi 69 kutoka nchini marekani huwa hawezi kukaa bila kumchokonoa mtu, maisha yake yamekuwa ya bifu na kutupiana maneno na watu mitandaoni kila uchao.
Kabla ya kumalizana na Meek Mill na Lil Durk, Tekashi amemvaa rapa Cardi B kwa madai ya kuwalewesha wanaume akitumia dawa za kulevya na kuwaibia hotelini kipindi cha nyuma.
Kama utakumbuka mwaka wa 2019 Cardi B aliwahi kukiri hadharani kwamba alikuwa akiwapa dawa za kulevya Wanaume na kuwaibia kwenye chumba hotelini kipindi anafanya kazi ya kuchojoa nguo (stripper) kwenye makumbi ya starehe.
Lakini mpaka leo hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yake.
Kwa mantiki hiyo ni kama Tekashi 69 anaendelea kumchokoza Cardi B ambaye amekuwa kimya.
Ikumbukwe mwezi Septemba mwaka wa 2019 Tekashi 69 alimtaja Cardi B kuhusika kwenye genge la kihuni maarufu kama Bloods Gang, kipindi anatoa ushahidi wake kwenye kesi iliyokuwa ikimkabili.