Zikiwa zimesalia wiki mbili tu kabla uchaguzi wa Chama cha Wafanyakazi wa Kaunti ya Trans Nzoia kufanyika, wawaniaji wa viti mbalimbali wanaendeleza kampeni huku baadhi yao wakiahidi kuboresha mazingira ya utendakazi kupitia mazungumzo na ushauriano na mwajiri.
Mwaniajia wa katibu mkuu wa chama hicho, Ronald Simiyu anasema ilivyo kwa sasa kuna pengo kuu baina ya washikadau hivyo kuchangia mizozo ya kisheria ya mara kwa mara.
Simiyu ambaye ameajiriwa katika kitengo cha kuzima moto na kukabili majanga kunti hiyo amesema atahakikisha kwamba kila mfanyakazi anawezeshwa kuhudhuria warsha ya kupokea mafunzo fursa inapopatikana, kwenda likizo na maslahi yao kufanywa kipaumbele.