Staa wa muziki nchini Uganda Kalifah Aganaga ametangaza kuja na album mpya mwaka huu.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook Aganaga amesema baada ya kushindwa kuachia nyimbo kali mwaka jana, sasa mwaka huu anakuja na album mpya ambayo itakithi vigezo vyote vya wapenzi muziki mzuri kutoka Afrika Mashariki.
Hata hivyo amesema mwaka wa 2020 alipoteza muda wake mwingi kwenye masuala ya siasa lakini sasa ameelekeza nguvu zake zote kwenye suala la kuwapa mashabiki zake muziki mzuri ambao wameukosa kwa muda.