Mastaa wa muziki wa Rap kutoka Nchini Marekani Meek Mill na Tekashi 69 karibu warushiane makonde baada kuingia kwenye mzozo mkali nje ya klabu moja huko Atlanta, nchini Marekani.
Rappers hao walikuwa kwenye sherehe katika Night club moja huko Atlanta kabla ya kukutana kwenye eneo la Maegesho ya Magari, ambapo wameonekana katika video wakipiga kelele na kutukanana wakati wakizuiwa na Walinzi wao.
Wawili hao wali-share clip za tukio hilo katika Mitandao yao ya kijamii na kila mmoja akijaribu kuelezea tukio hilo kwa upande wake.
Ikumbukwe Meek Mill na Tekashi 69 wamekuwa katika bifu kwa miezi kadhaa sasa baada ya Meek mill kumuita tekashi ‘Panya’ katika chapisho lake la mwezi mei mwaka wa 2020 katika mtandao wa twitter.