Msanii wa muziki kutoka pande za Kitale kaunti ya Trans-Nzoia , Iyanizzo ametangaza kuachia ep yake Ijumaa hii kama zawadi ya valentines kwa mashabiki zake.
Akipiga stori na North Rift Radio mkali huyo wa ngoma ya “Title Deed” amesema EP hiyo ameipa jina la salad ep na itakakuwa na jumla ya ngoma 6 ambayo imetayarishwa na maprodyuza mbali mbali kuleta ladhaa ya muziki mzuri.
Hata hivyo Iyannizo amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kwani ataachia rasmi salad EP Februari 5 mwaka wa 2021.