GOOGLE KUFANYA MABADILIKO KATIKA MFUMO WAKE WA MATANGAZO

You are currently viewing GOOGLE KUFANYA MABADILIKO KATIKA MFUMO WAKE WA MATANGAZO
  • Post category:Teknolojia

Google imetangaza wiki hii kuwa itafanya mabadiliko katika mfumo wake wa matangazo. Mtandao huo umesema utaacha rasmi kusambaza matangazo yake kuendana na historia ya kuperuzi katika website mbalimbali unazotembelea na kuanzia mwakani inapanga kutumia mfumo mpya wa kusambaza matangazo bila kutegemea cookies na trackings.

Kikawaida Google inashirikiana na websites na site nyingi kukusanya historia ya watumiaji ili kukupatia matangazo yanayoendana na unachofuatilia. Kwa mfano ukitazama website za vyakula, ni rahisi kupewa matangazo ya vyakula, ukitazama sana website za magari, ni rahisi kuona matangazo ya Magari.

Google imesema matangazo yote kuanzia mwakani yatakuwa yanatokea kwa kila mtu bila kufuatilia data zako huku ikitoa ahadi ya kufunga uwekezaji wake na tafiti za Ad-tracking.

Google imejiwahi mapema baada ya Apple na Mozilla kuthibiti mifumo ya kutrack watu wanavyoperuzi mitandaoni.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa