GAVANA NANOK AFANYA MABADILIKO MADOGO KWENYE SERIKALI YAKE

Gavana wa kaunti ya Turkana Josphat Koli Nanok amefanya mabadiliko madogo kwenye nyadhifa za baadhi ya maafisa wakuu katika serikali yake.

Nanok amemteuwa aliyekuwa Afisa mkuu katika Wizara ya Utalii,Utamaduni na Mali Asili Rosemary Nchinyei kuwa Afisa mkuu mpya katika Wizara ya Barabara na Uchukuzi akishikilia pia wadhfa wa afisa mkuu katika Idara ya Kazi ya Umma japo kikaimu.

Wakati huo huo aliyekuwa Afisa  mkuu katika Wizara ya Barabara na Uchukuzi John Ariko Namoit  ameteuliwa kuwa Afisa mkuu katika Wizara ya Utali,Utamaduni na Mali Asili.

Hata hivyo Gavana Nanok amesema  kuwa mabadiliko hayo ni katika hali ya kuboresha huduma kwa wananchi wa kaunti ya Turkana huku akiahidi mabadiliko zaidi.

Robert Elim

Presenter and News Editor at North Rift Radio Kenya