GEREZA LA NGERIA KAUNTI YA UASIN GISHU LAPOKEA MSAADA WA VITAMVUA KUPAMBANA NA JANGA LA CORONA

Wafanyikazi na wafungwa katika gereza la Ngeria viungani mwa mji wa Eldoret kaunti ya Uasin Gishu wamepokea msaada wa barakoa kutoka kiwanda cha Rivatex kama njia moja ya kuzuia maambukizi ya virusi vya korona.

Akizungumza na wanahabari baada ya kuwapokeza msaada huo Mkurugenzi mkuu wa kiwanda hicho Profesa Thomas Kipurgat amesema wao kama taasisi ya serikali watahakikisha wanakua kie elezo kusaidia kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona.

Kwa upande wake Afisa anayesimamia gereza hilo Joseph Saitoti ameelezea furaha yake kutokana na msaada huo anaosema utawasaidia pakubwa kwani wengi wa wafanyikazi na wafungwa walikuwa bado kupata bidhaa hiyo muhimu.

Robert Elim

Presenter and News Editor at North Rift Radio Kenya