EX WA MCHEKESHAJI ERIC OMONDI-CHANTEL AMTAMBULISHA BOYFRIEND WAKE MPYA 

EX WA MCHEKESHAJI ERIC OMONDI-CHANTEL AMTAMBULISHA BOYFRIEND WAKE MPYA 
  • Post category:Burudani

Mrembo Chantal Juliet Grazioli hayupo tena sokoni kwani  amepata boyfriend mpya.

Chantal alikuwa girlfriend wa mchekeshaji humu nchini Eric Omondi. Wawili hao waliachana mwaka 2018, miaka miwili baada ya kuchumbiana.

Hawajawahi kueleza sababu ya kufanya hivyo japo wameendelea kuwa marafiki hadi sasa na Eric amekuwa akiweka comments mara kadhaa kwenye picha za ex wake huyo.

Kupitia Instagram wiki iliyopita, Chantal aliweka picha akiwa na boyfriend wake mpya na kuweka emoji za ‘malavidavi’ pasipo maelezo mengine.

Mashabiki wa mrembo huyo wameonekana kumkubali shemeji yao mpya.

“Now that’s your kind of guy,” ameandika shabiki mmoja na kuongeza, “we can clearly see the love,as of what’s his face Eric who, hangemake.”

Robert Elim

Presenter and News Editor at North Rift Radio Kenya