Mchekeshaji wa humu nchini Eric Omondi ametia nia ya kutaka nafasi ya ubalozi wa sekta ya utalii nchini.
Wadhfa huo ambao juzi kati ulipewa mwanamitindo wa Uingereza Naomi Campbell, utahusisha kutangaza Kenya kama kituo cha utalii kimataifa.
Omondi ameshare ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akielezea ni kwanini anafaa apewe kazi hiyo, huku akitoa mfano wa matukio mbali mbali ambayo ameyatangazia Kenya kimataifa bila malipo yoyote.
Aidha ameenda mbali zaidi na kumpendekeza mshindi wa tuzo ya Oscar, Lupita Nyong’o kuteuliwa kama naibu wake kwenye wadhfa wa ubalozi wa utalii.
Hata hivyo Eric Omondi amedokeza kwamba ana mpango wa kukutana na Waziri wa Utalii nchini Najib Balala kujadiliana kuhusu suala hilo.