Mwanamuziki kutoka nchini Uganda DJ slick stuart amekana madai yanayosambaa mitandaoni kuwa alirushiana makonde na Chosen Blood kwa sababu ya penzi la Winnie Nwagi.
Akiwa kwenye moja interview msanii huyo ambaye pia ni DJ amesema yeye na Chosen Blood ni washikaji wa muda mrefu na hakuna vile wanaweza pigana kwa sababu ya mwanamke huku akienda mbali zaidi na kusema kwamba hawajeona na wasanii Winnie Nwagi na Chosen Blood kwa muda sasa.
Hata hivyo amekana kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na msaani winnie nwagi huku akisema wanaoneza uvumi huo wanataka kumharibia brand yake ya muziki.
Kauli ya Dj Slick Stuart inakuja mara baada ya watu kwenye mitandao ya kijamii kudai kwamba alipigana na Chosen Blood kwenye moja ya night club huko Kampala kwa sababu ya penzi la Winnie Nwagi.