WILLY PAUL ATOA YA MOYONI KUHUSU TASNIA YA MUZIKI NA FILAMU NCHINI.

You are currently viewing WILLY PAUL ATOA YA MOYONI KUHUSU TASNIA YA MUZIKI NA FILAMU NCHINI.
  • Post category:Burudani

Staa wa muziki nchini Willy Paul ameonyesha kuumizwa na jinsi ambavyo wasanii wa humu nchini wanaendelea kutaabika mikononi mwa watu wachache ambao wanapora pesa zao.

Mkali huyo wa ngoma ya “Nomare” amesema vijana wengi nchini ambao wana talanta kwenye tasnia ya muziki na filamu wanaendelea kuumia kwa sababu ya watu wachache ambao wamepewa majukumu ya kusimamia pesa za wasaani.

Kauli ya Willy Paul inakuja mara baada muigizaji wa kipindi cha “Tahidi High” Joseph Kinuthia maarufu kama Omosh kuweka wazi matatizo anayoyapitia kwenye moja ya video inayosambaa mitandaoni huku akionekana akiomba msaada kutoka kwa wahisani kwani amefilisika kiuchumi.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa