WEEZDOM APATA KIGUGUMIZI JUU YA KURUDIANA NA EX WAKE MYLEE STAICEY.

You are currently viewing WEEZDOM APATA KIGUGUMIZI JUU YA KURUDIANA NA EX WAKE MYLEE STAICEY.
  • Post category:Burudani

Aliyekuwa msanii wa lebo ya muziki ya EMB Weezdom ameshindwa kuweka wazi kama kuna uwezekano wa kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake Mylee Staicey ikiwa ni miezi kadhaa  sasa baada ya mahusiano yao kuvunjika.

Akijibu swali la shabiki yake aliyetaka msanii huyo arudiane na mrembo huyo kwenye mtandao wa Instagram Weezdom  amesema hajui kile ambacho mungu amempangia katika maisha, hivyo hawezi jiamulia mwenyewe.

Mkali huyo wa ngoma ya “Better Man” amekana madai yanayotembea kwenye mitandao ya kijamii kuwa aliyekuwa mpenzi wake Mylee Staicey alitoka kimapenzi na dansa mmoja nchini, hivyo kupelekea mahusiano yao kuvunjika.

Na katika post tofauti kwenye mtandao wa Instagram Weezdom ambaye ni meneja wa msanii Kevin Bahati amedinda kumtambulisha baby mama wake na mwanae kwa umma mara baada ya kupata shinikizo kutoka kwa mashabiki zake.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa