DADDY OWEN AZIDI KUANIKA MASAIBU YA NDOA YAKE NA MKEWE.

You are currently viewing DADDY OWEN AZIDI KUANIKA MASAIBU YA NDOA YAKE NA MKEWE.
  • Post category:Burudani

Mwanamuziki Injili nchini Daddy Owen ameendelea kufunga sababu zilizopelekea ndoa yake na mkewe Farida Wambui kuvunjika.

Akipiga stori na Gazeti moja nchini Daddy Owen amesema masaibu ya ndoa yake yalimpelekea kupata msongo mawazo ambao ulikuwa unafanya ajifungia chumbani na kulia.

Hitmaker huyo ngoma ya Vanity amesema jambo hilo lilimuathiri kimuziki kwani alisitisha shughuli zote za kuandika na kutoa nyimbo ikizingatiwa kuwa kila kitu maishani kilikosa umuhimu.

Duru zinasema kuwa Daddy Owen na mkewe Faridah wapo kwenye mapambano ya kisheria huku ikielezwa kwamba mkewe huyo amemtaka Daddy Owen aondoe picha zake na watoto wao kwenye kurusa zake za mitandao ya kijamii.

Sanjari na hilo Daddy Owen amedokeza kwamba huenda akafuata ushauri wa msanii mwenzake Emmy Kosgei wa kusafiri nje ya nchi hadi pale stori za ndoa yake na mkewe kuvunjika zitakaposahaulika

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa