Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Pia Ponds amekiri kuwa kuna kipindi karibu aache muziki baada ya watu kumshambulia na matusi kwenye mitandao ya kijamii.
Akiwa kwenye moja ya Interview Pia Ponds amesema uongozi wa lebo ya muziki ya Big Talent ulimshauri jinsi ya kukabiliana na matusi ambayo alikuwa akipokea kutoka kwa mashabiki wake.
Aidha amesema licha ya muziki wake kubezwa na baadhi ya wadau wa muziki nchinin Uganda anaamini kwamba kuna siku muziki wake utakubalika kote duniani.
Ikumbukwe kwa miaka kadhaa sasa Pia Pounds amekuwa akishambulia kwenye mitandao ya kijamii lakini inaonekana amezoea hali hiyo.