Ukitaja wakongwe wa muziki wa Taarab huwezi kumuacha marehemu Bi.Kidude ambaye ni moja kati ya wanamuziki waliowavutia watu wengi sana, rapa Country Boy kutoka Tanzania ni moja ya watu wanaovutiwa na marehemu Bi.Kidude .
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Country Boy ameweka wazi kuwa ana mpango wa kuachia albam yake mwaka huu na anatamani kutumia picha ya Bi.Kidude kama cover ya albam hiyo.
Tuna imani kama ataamua kuitumia picha ya mkongwe huyo kama cover ya albam yake, basi atafuata utaratibu kama inavyotakiwa ili kuitumia picha hiyo.