Staa wa muziki wa Dancehall kutoka nchini Uganda Cindy Sanyu amejipata pabaya baada ya mashabiki wa muziki nchini humo kumshambulia kwenye mitandao ya kijamii.
Hii ni baada ya msanii huyo kuweka wazi kwamba ili afanye collabo na msanii yeyote chipukizi anahitaji shillingi laki 1.5 kama malipo.
Sasa kauli hiyo ya Cindy imeonekana kuwakera baadhi ya wadau wa muziki nchini Uganda ambao wameenda mbali zaidi na kumtaka msanii huyo aache suala la kuwatoza pesa wasanii chipukizi na badala yake awasaidie kimuziki kama namna ambavyo wasanii wengine wakubwa nchini humo wamekuwa wakifanya.