Msanii nguli wa muziki nchini Uganda Jose Chameleone ambaye juzi kati aliwania wadhfa wa umeya wa jiji la Kampala ameahidi kuachia album yake mpya kama njia ya kutangaza kuwa bado yupo kwenye biashara ya muziki.
Akiwa kwenye moja ya Interview mkali huyo wa ngoma ya Bolingo ya Nzambe amesema kwa sasa yupo kwenye harakati za kuifanyia kazi album yake mpya akiwa pamoja na maprodyuza mbali mbali, hivyo mashabiki wake watarajia kuipata album hiyo hivi karibuni.
Hata hivyo amewaondolea hofu mashabiki zake kwa kusema kuwa atabaki kuwa mwanamuziki milele na hata ikitokea amefuata ndoto zake za kuwa mwanasiasa.